Spacer

 

Google Translate

IPEN

A Toxics-Free Future

Donate

AGENDA Waungana Na TGNP Mtandao Kuelimisha Jamii Athari Za Madini Zebaki (Mercury)

https://habari24.blogspot.com/2017/06/agenda-waungana-na-tgnp-mtandao.html

vicent macha 

Watanzania wametakiwa kuepuka na kuachana na matumizi ya Zebaki (Mercury) kwenye maisha yao ya kila siku kwani madini hayo ni hatari kwa vizazi vya sasa na baadae. Hayo yamezungumzwa mapema leo kwenye semina iliyofanyika ofisi za Mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP) ikiwa na wawezeshaji toka Agenda for Enviroment and Responsible Development.

Afisa program Mkuu wa Agenda Mr. Silvani Mng'anya akitoa ufafanuzi juu jambo mapema leo jijini Dar es salaam.

Akitoa mawasilisho hayo kwa wanaharakati na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam afisa mkuu wa programu agenda Mr Silvani Mnganya alisema kuwa watanzania inabidi tuachane na matumizi ya zebaki na kuangalia mbadara wake katika kila sehemu ambayo ilikuwa ikitumika kwa faida zetu na jamii kwa ujumla.

Alisema watu wengi tunatumia au tunawekewa bila wenyewe kujua madhara yake kwa baadae. Zebaki ni dawa na hutumika kuzibia meno yaliyotoboka ambayo kitaalamu huitwa (Dental Amalgam).

lakini pia hutumiwa na wachimbaji wa dhahabu na makaa ya mawe kwa kichoma na inapochomwa moshi wake ni hatari kwani yenyewe inasambaa kwa njia ya hewa hivyo huathiri viumbe vyote vinavyovuta hewa hiyo.

Vipodozi wanavyotumia wanawake kuchubua Ngozi vingi huwa vina madini ya Zebaki mfano sabuni ya Jaribu na Ricco ambazo zilikatazwa na serikali kwani ni hatari kwa ngozi zao na pia kusababisha magonjwa kama kansa na mengineyo.

Baadhi ya vifaa vinavyotumika hospitalini na Mahabara za Mashuleni kama Barometa, vipima joto na kifaa cha kupimia shinikizo la damu (Sphygmomanometer) vinamadini ya Zekaki hivyo huathiri watumiaji.

Vingine ni Betri, Swichi na Taa za umeme, Swichi za Redio na baadhi ya dawa za kuulia wadudu vimetengenezwa na madini hayo.

Alisema zebaki huingia kwenye mazingira kutoka kwenye miamba yenye madini hayo shuguli za kibinadamu kama Viwanda vinapomwaga kemikali za zebaki ambazo huingaia Baharini, Mtoni Ziwani na sehemu nyinginezo wananchi wakinywa yale maji au kula viumbe wanaopatikana mule kama Samaki hupata athari hizo.

Kuchoma Makaa ya Mawe au takataka za aina nyingi bila kujua ndani kama kuna vitu vimeundwa na madini hayo hivyo moshi uingia watu na kuwapa madhara.

Lakini pia kwa wale watu wenye utaratibu wa kuchoma maiti kama Indu na jamii kubwa ya watu toka Asia kama aliyekufa alizibwa jino au meno basi ule moshi sio mzuri kwa afya za wananchi wa maeneo ya karibu.

Afisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Pamoja TGNP Anna Sangai akiongoza semina iliyofanyika ya makao Makuu ya Mtangao wa Jinsia Tanzania

Lakini tukiachana na hayo yote zebaki ina madhara makubwa yafuatayo.

Inasababisha madhara hasi kwa uzazi kuharibu mbegu za kiume, kusababisha kasoro kwa watoto wanaozaliwa ,kuharibika kwa mimba kwa mtoto wa kike inapunguza maendeleo wakati wa mimba na katika kipindi cha utoto.

Inaharibu mfumo wa kuona na kusikia, kutetemeka kwa mwili na kukakamaa kwa misuli, kupooza ugonjwa wa kukosa usingizi na kuleta udhaifu wa kihisia.

Inasababisha matatizo ya mishipa ya fahamu hasa hasa kwa wanawake ambao ndio wako katika umri wa kuzaa.

Inasababisha uharibifu wa vina saba.

Inasababisha mzio unaoleta vipele kwenye ngozi, kuchoka na maumivu ya kichwa.

Inapunguza uwezo wa watoto kufikiri au kuweka kumbukumbu.

Hivyo basi mnamo mwaka 2013 nchi ya japani ikiwa ni mwenyeji iliungana na nchi nyingine 56 kuweza kuunda mkataba wa MINAMATA ambao ulikuwa na lengo la kupunguza ikiwezekana kuondoa kabisa matumizi ya Zebaki katika nchi wanachama. Na kwa sasa nchi hizo zimefikia 128 Tanzania ikiwemo katika nchi wanachama kwa kuwa ilionekana nchi zinazoendelea ndizo zinatumia sana madini haya katika shughuli zake.